Jumatano , 22nd Jun , 2022

Mabehewa sita ya Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora  mpaka Dar es salaam yameanguka katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika manispaa ya Tabora

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora ACP. Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi linaendelea  kufuatilia kutokana na  abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya matibabu.


Aidha amesema chanzo cha ajili hiyo mpaka Sasa bado hakijulikani na ufuatiliaji bado unaendelea.

#UPDATES 

Watu wanne wakiwemo watoto wawili wamefariki na wengine 132 wakijeruhiwa katika ajali ya Treni ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma kwenda Dar es salaam 

Taarifa ya TRC imeeleza kuwa Treni hiyo ilitoka Kigoma Juni 21 saa mbili usiku na imepata ajali eneo la Malolo mkoani Tabora leo Juni 22/2022 saa tano asubuhi