Ijumaa , 13th Mei , 2022

Watu wanne wa familia moja  wakazi wa kijiji  cha Kilino  kata ya Isanzu Wilayani Nzega Mkoani Tabora wamejeruhiwa vibaya  na Fisi maeneo  mbalimbali ya miili yao  wakati wakiwa shambani wakinyunyuzia dawa katika  mimea ya pilipili hoho  

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP. Richard Abwao amesema Fisi huyo ambaye alizuka kutoka mahala pasipo julikana aliwavamia wanafamilia  hao waliokuwa wakiendelea na shughuli zao shambani na kuwararua vibaya  maeneo mbali mbali ya miili yao hasa  katika upande wa mikono yao .

Kamanda amesema wakazi wa eneo hilo wamefanikiwa kumuua Fisi huo, huku  hali ya majeruhi ikitajwa kuendelea vizuri  baada ya kukimbizwa Hospitali  kwa ajili ya matibabu .