
Wito huo umetolewa Februari 14, 2024 wakati wa zoezi la ugawaji wa fomu kwa kwa baadhi ya wanachama waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Chama, Mwenyekiti wa Chama, Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama.
Aidha, Ndugu Bashange amebainisha kuwa kwasasa wanawake wamepewa nafasi kubwa ya kuwania nafasi za uongozi ambapo katika Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu wawili watachaguliwa, mmoja atakuwa ni mwanamke.
Zoezi la kuchukua fomu limeanza leo tarehe 14 February na litatamatika hadi kufikia 29 Feb ambapo utafanyika mkutano wa Uchaguzi ambapo katika zoezi hilo wenyeviti na makatibu wa mikoa 27 wamemchukulia fomu ya kugombea Uenyekiti wa Taifa Mhe. Otham Masoud Othman.