Mshauri wa jinsia wa Shirika la Plan International Bi. Jane Mrema
Wananchi hao kutoka katika vijiji vya msia, kinambo, kisa na milepa wengi wao wakiwa ni wahudumu wa afya vijijini , wamesema wakati umefika badala ya wanaume kuwaacha wake zao kuyachukua matokeo ya vipimo vya afya walivyopima na kuvifanya ni vya yao pia,
Aidha Wananchi hao wameongeza kuwa Wanaume kwa sasa wanapaswa wawasindikize wenza wao wakati wote wa ujauzito na kupima afya na tabia hiyo iwe endelevu na sio wakati wa Ujauzito tu
Akiongea na wananchi hao , Mshauri wa jinsia wa Shirika la Plan International Bi. Jane Mrema, ametoa wito kwa wanaume wote waliobadilika na kuukimbia mfumo dume ndani yao, wasifanye hivyo wakati wenza wao wakiwa wajawazito pekee, bali wafanye usaidizi huo kuwa endelevu kwa ajili ya kuwapunguzia wanawake mzigo.




