
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Ngonyani Msongozi
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kufika kwenye kituo cha afya mkoa wa Ruvuma na kuchoma chanjo ya Uviko-19, na kusema kwamba suala la nguvu za kiume linaletwa na lishe bora na sio kwa walaji wa chipsi mayai asubuhi hadi jioni.
"Wanaume wengi wamekuwa wakipotosha wanadai kwamba watu wakichanja basi mawasiliano ya 'White house na Black house' yatakuwa yamekatika, nendeni mkachanje, pateni lishe zingatieni kanuni mwanaume lazima upate chakula kizuri uwe na afya njema unaweza ukawa unakula chips mayai asubuhi hadi jioni kweli unaweza kuwa mwanaume bora, lazima utakuwa na shida," amesema Mbunge Msongozi.