Jumatatu , 26th Sep , 2022

Watoto watatu kati ya watoto wanne raia wa Canada wa wazazi Bi.Edith na Bw.Sébastian ambao wamekutwa na ugonjwa wa kinasaba ambao utawafanya wapofuke macho muda wowote, wamelazimika kuwasafirisha watoto wao duniani ili kupata taswira ya mengi yaliyopo duniani kabla watoto hao hawajapofuka.

 

Hali hiyo kitaalamu inaitwa Retinitis pigmentosa , hali ambayo mtu huzaliwa akiwa nayo na haina dalili zozote. 

Familia hiyo inaendelea kusafiri duniani, na sasa ikiwa huu ni mwezi wa sita wa safari yao kati ya miezi 12 waliojipangia kusafiri ambapo tayari wameshatembelea nchi za  Namibia, Zambia, Tanzania, Uturuki, Mongolia na Indonesia.