Jumapili , 6th Apr , 2014

Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Frederick Sumaye amesema wanasiasa wanaousaka urais ndio wamekuwa chanzo cha vurugu na machafuko katika nchi nyingi barani Afrika.

Sumaye amesema hayo jana kwenye chuo kikuu cha Wesley nchini Marekani wakati akiwasilisha mada kuhusu wajibu na ushiriki wa mwanamke katika kueneza amani na michakato ya maamuzi barani Afrika.

Waziri mkuu huyo mstaafu amefafanua kuwa baadhi ya vurugu na machafuko vimesababisha viongozi kuondolewa madarakani na hata wengine kuuwawa huku akiitaja sababu nyingine kuwa ni utawala mbovu unaochochea maovu kama rushwa na kubebana.