Jumatatu , 1st Feb , 2016

Hayo yamesemwa Bungeni Dodoma katika kikao cha Bunge ambapo naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maend

Hayo yamesemwa Bungeni Dodoma katika kikao cha Bunge ambapo naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamis Kigwangalla alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum CCM Faida Mohamed Bakari.

Mbunge Farida ametaka kujua namna serikali ilivyojipanga kutokomeza tabia mbaya ya wahudumu wa afya hasa kutoa lugha chafu kwa wagonjwa hususani kwa kinamama wajawazito.

''Ni marufuku kwa wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na wana bodi zao za taaluma zao hivyo kila mgonjwa anaehudumiwa aangalie anahudumiwa na nani na atoe maoni yake katika eneo husika ili sheria ichukue mtandao wake'' Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Aidha Dkt. Kigwangalla amesema wizara yake pia imeandaa utaratibu maalum wa kutoa semina kwa wakunga wa jadi ili waweze kutoa huduma vijijini kwa utaratibu utakao leta tija zaidi.