
Mary Chatanda Mwenyekiti wa UWT Taifa
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Igaga Wilaya ya Kishapu Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema watoto wanapomaliza darasa la saba ambao watashindwa kufaulu wazazi wasikimbilie kuwaozesha na kuwataka kuwapeleka vyuo vya ufundi stadi.
Amesema kuna baadhi ya wazazi wanatamaa ya kupata mali haraka wanaamuwa kuozesha watoto wao ambao bado wako shule jambo ambalo halikubaliki kwani ni kumnyima mtoto haki yake ya kupata elimu.
“Mtoto anapomaliza shule ya msingi na kwa bahati mbaya akafeli msikimbilie kumuozesha sasa hivi serikali imejenga vyuo vya ufundi stadi kila Wilaya wapelekeni watoto wakapate ujuzi ambao utawasaidia katika maisha yao pia na wazazi mtanufaika”amesema Mary Chatanda Mwenyekiti wa UWT Taifa
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari akizungumza na wakazi wa Kata ya Maganzo na Idukilo amekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika kuanzia ngazi ya familia huku baadhi ya wanawake wakifumbia macho bila kutoa taarifa.
“Wanawake nyinyi ni jeshi kubwa mnapoona kuna vitendo vya ukatili vinafanyika toweni taarifa acheni kumaliza kesi hizo ngazi ya familia,pia muwalee watoto wenu kwa kuzingatia maadili na kuepuka kuiga tamaduni za kigeni” amesema Zainab Shomari Makamu Mwenyekiti UWT Taifa