Jumatatu , 8th Dec , 2014

Wananchi zaidi ya 200 wanaondolewa kupisha hifadhi ya pori la akiba la Mpanga Kipengele katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha baada ya kutelekezwa bila kulipwa fidia zao kwa zaidi ya miaka 8 sasa.

Wakazi wa kitongoji hicho wamesema kwa sasa wote wanaishi kwenye vijumba na matembe yaliyojengwa kwa miti, udongo na kuezekwa kwa nyasi na maturubai, wanasema yanaweza kuanguka muda wote.

Mkuu wa wilaya ya Mbarali Bwana Gulam Husein kifu amekiri kuchelewa kwa fidia hiyo na amesema serikali inaendelea kushughulikia na kwamba malipo yao yatakuwa tayari mwanzoni mwa mwaka 2015.

Baadhi ya wadau na asasi za kiraia, wamesikitishwa na ucheleweshwaji wa fidia hiyo, ambapo wamesema huko ni kukwamisha maendeleo ya wananchi.

Hivi karibuni waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu alisema serikali inachukua hatua kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya ya mbarali ili kuhakikisha suala hilo linakamilishwa .

Sheria ya ardhi namba 4 na namba 5 ya mwaka 1999 inasema fidia kamili na ya haki italipwa kwa mmiliki wa ardhi bila kuchelewa pale tu ardhi yake inapotwaliwa na serikali kwa manufaa ya umma.