Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Prudenciana Protas akizungumza na waandishi hawapo pichani.
Kutokana na vitendo vya uhalifu na mauaji kundelea kushamiri katika Kata hiyo uongozi wa Kata hiyo umelazimika kuwakutanisha wananchi wa Kata na uongozi wa Jeshi la Polisi wilaya ili kutoa malalamiko yao.
Wakizungumza kwa hisia kali wananchi wa Kata hiyo akiwemo Diwani wao Reginald Danda, mbele Mkuu wa Polisi wilaya ya Njombe, Msolo H Msolo, wamesema baadhi ya wahalifu katika vijiji vya Kata hiyo wamefikishwa polisi zaidi ya mara kumi na kuachiwa huru.
Malalamiko haya ya wananchi hao yameongezewa nguvu na Diwani wa Kata hiyo Reginald Danda, ambaye naye analalamikia ushirikiano mdogo dhidi ya vitendo vya jeshi la polisi kuwaachilia wahalifu kwa kupewa rushwa.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Njombe Msolo H Msolo, akiwa katika mkutano huo amekanusha Jeshi la Polisi kuhusika kuwakumbatia wahalifu na badala yake amesema wanasheria wa mahakama ndio chanzo cha kuachiwa huru watuhumiwa.
Kwa Kata ya Iwungilo pekee ndani ya Halmashauri ya mji wa Njombe katika kipindi cha tangu mwezi Januari hadi Mei mwaka huu zaidi ya pikipiki 20 za miguu miwili zimeibiwa pamoja na kutokea matukio matano ya mauaji wakati wa wizi huo.