
Awali akifungua Mkutano Mwenyekiti huyo ameanza kwa kuwataka wananchi kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo ili waweze kufikia malengo yao ya mafanikio na hatimaye anatamka kauli inayo washitua wananchi ya kutaka kujiuzulu nafasi hiyo.
Licha ya mwenyekiti wa kijiji hicho kusita kueleza chanzo cha cha kutaka kujihuzulu nafasi hiyo wananchi wa kijiji katika mkutano huo wakasema hakuna haja ya kuficha ukweli kwani wao wanajua chanzo cha kiongozi wao huyo kutaka kuachia ngazi ni kuenguliwa kwenye kamati ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata unao endelea kutekelezwa kijiji hapo.
Kutokana na hali hiyo kituo hiki kimelazimika kumtafuta diwani wa kata ya Iwungilo ili kujua ukweli juu ya kuondolewa kwa mwenyekiti wa kijiji cha Iwungilo kwenye kamati hiyo kama wananchi walivyoeleza katika mkutano.