Ijumaa , 7th Mei , 2021

Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini Joseph Musukuma, amesema kuwa asilimia 92 ya jimbo lake limezungukwa na Ziwa Victoria lakini wananchi wake wanakunywa maji machafu hali inayopelekea kuugua kichocho.

Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini Joseph Musukuma

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 7, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maji iliyowasilishwa hapo jana na Waziri wa Wizara hiyo Jumaa Aweso, ambapo amemtaka Waziri huyo mara baada ya Bunge hilo kuisha ahakikishe anaongozana naye kwa ajili ya kuzindua miradi ya maji katika vijiji alivyomuahidi.

"Asilimia 92 ya jimbo langu ni Ziwa lakini sisi tunaugua kichocho, tunachota maji machafu halafu maji yamevutwa yameletwa mpaka Dodoma, Waziri nikuombe sana 'term' hii usinizingue tumekuwa wavumilivu vya kutosha uone namna yoyote hii uje ufungue miradi ya maji kwenye vijiji ulivyoniahidi", amesema Mbunge Musukuma.