Alhamisi , 17th Nov , 2016

Mipango ya serikali ya kuifikisha Tanzania kuwa taifa la uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 inaweza kufanikiwa iwapo wanahabari nchini watakuwa na uelewa wa kutosha wa kuripoti habari za uchumi hasa zile zinazolenga kuisaidia serikali kufikia malengo

Dkt. Blandina Kilama

Mtafiti Mwandamizi kutoka taasisi ya utafiti wa kupunguza umaskini ya (REPOA) Dkt. Blandina Kilama amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya uchumi kwa wanahabari wanaohusika na uandishi na utangazaji wa habari za uchumi na biashara.

Dkt. Kilama amesema kuna maeneo mengi ambayo iwapo wanahabari watayafahamu, yatawawezesha kuwa kiunganishi kati yao na wananchi kwa upande mmoja na kwa upande mwingine kati yao na taasisi za utafiti wa uchumi ikiwemo REPOA pamoja na serikali, wa jinsi machapisho na taarifa za kitaalamu zinavyoweza kusaidia katika kufikia malengo hayo ya kiuchumi.