
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
Simbachawene ametoa agizo hilo leo Agosti 6, 2021 Jijini Dar es Salaama mara baada ya kuiona video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha kundi la watu wakiwavamia wapenzi hao na kuwadhalilisha kwa kuwapiga na kuwarushia maneno.
"Hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu ambao wanawavamia na kuingia katika maeneo ambayo watu wenye mahusiano ya kimapenzi wanakwenda kufanya faragha zao tabia hii ambayo imeshamiri sasa kama ambavyo clip nyingi zimekuwa zikirushwa rushwa nadhani leo nichukue nafasi kutoa msimamo wa kisheria na kukemea tabia hii ambayo imeanza kuota mizizi," amesema Waziri Simbachawene.