
Akiwa katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma katika ukaguzi wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya shule za msingi (BOOST) mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomasi amesikitishwa na usimamizi mbovu wa ujenzi wa matundu 14 ya vyoo katika shule hiyo iliyopo kata ya Mtipwili wilaya ya Nyasa mkoni Ruvuma
Ujenzi huo uligharimu kiasi cha shilingi milioni 36 ambapo mkuu wa mkoa wa Ruvuma ameagiza kukamtwa na kufanyiwa uchunguzi wasimamizi wote ambao wameshindwa kusimamia mradi huo.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Mtipwili wamesema kitendo cha kushindwa kusimamia mradi huo ni kibaya na licha ya serikali kutoa milioni 36 katika ujenzi wa matundu 14 ya vyoo vya shule hiyo lakini pia wananchi walichangishwa kiasi cha shilingi elfu 5 kwa kila kaya pamoja na kuchimba mashimo ya vyoo hivyo