Virusi vya Corona
Kauli hiyo ameitoa leo Machi 6, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani humo na kuzitaka mamlaka husika, kusitisha uingiaji wa ndege za wageni kutoka nchini Italia kwa kipindi hiki hadi Serikali itakapojipanga.
"Hapa Zanzibar hatuna ugonjwa wa Corona na upotoshwaji juu ya hizi taarifa naviomba vyombo husika viwachukulie hatua madhubuti kwa watu wanaotoa taarifa zisizo sahihi, kuna ndege zetu za watalii kutoka Italy, tunawaambia waache kuja sasa hivi" amesema Waziri Mohammed.

