Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Mhe. Samia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika futari iliyotolewa kwa ajili ya watoto yatima zaidi ya 200 kutoka katika vituo vitano Jijini Dar es Salaam, amesema watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wanatakiwa kulindwa kwa kuwa ni nguvu kazi na viongozi wa baadae.
Makamu huyo wa Rais amesema kuwa inatakiwa kuwa na mipango Kabambe,ili kuwalinda lakini pia watu wenye uwezo na walio katika mazingira bora wawasaidie watoto hao ili kuwapa mwanga wa maisha yao ya baadaye.
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa amewataka waislam kutenda matendo mema katika jamii huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa wale wote watakohitaji kusaidia jamii katika kutatua matatizo tofauti.