Moja ya Ofisi za Chama cha Walimu Tanzania CWT.
Akizungumza wakati wa kufungua warsha kwa maofisa wa elimu wa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya mtendaji mkuu wa wakala wa mafunzo ya uongozi wa elimu
Amesema kuwa elimu hiyo italenga wakuu wote wa shule za msingi hapa nchini ambao utatolewa kwa ngazi ya cheti kwa walimu 800 kwa awamu ya kwanza kwa halmashauri nane za mikoa hiyo.
Masanja amesema kuwa elimu hiyo inafadhiliwa na mfuko wa kuwasaidia watoto duniani (UNICEF) na kuwa waalimu katika awamu zote tatu watalipiwa ada na kuwa masomo hayo yatatolewa kwa mfumo wa masomo ya mali (Distance leaning).
Amesema kuwa katika kila awamu kutakuwa na muda wa mwaka mmoja na kuwa kosi hiyo itakuwa na masomo 11 ambapo kutakuwa na wawamu tatu, na kuwa awamu hii itakuwa ni ya nyanda za juu pekee na kuwa katika mikoa mingine waalimu wanasoma kozi hiyo kwa sasa inaendelea mikoa Dar es Salaam na Mwanza.
Akuwa kuna waalimu wengine hawatakuwa wameingizwa katika mpango wa kulipiwa ada watatakiwa kulipa ada ya shilingi 500,000 kwa mwaka.
Amesema kuwa haizuriliwi kwa mwalimu ambaye hata chaguliwa kuingiza katika mfumo wa ufadhili wa Unicef na kuwa waalimu wakuu watateuliwa wale wenye diploma, na kuwa waalimu hatakama watakuwa na elimu zaidi ya diploma wataruhusiwa kusoma kwa kuwa elimu hiyo inalenga kusimamia elimu.
Walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wameaswa kujijengea mazoea ya kupenda kujiendeleza kimasomo hususani katika suala la utawala ili kuimarisha ufanyaji kazi hususani katika kuimarisha mahusiano katika tasnia ya elimu kwa ujumla.