Jumanne , 27th Sep , 2022

Serikali ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, imerusha cheche za kuwaonya walimu ambao wamekuwa wakiingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi hata wakati mwingine kuwasababishia ujauzito.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kaliua, Michael Nyahinga

Katika uzinduzi wa miongozo mitatu mahususi ya uboreshaji wa elimu kwa wilaya ya Kaliua, akizungumza Katibu Tawala wa wilaya hiyo Michael Nyahinga, kwa niaba ya  Mkuu wa wilaya amesema pamoja na miongozo hiyo kuwa na mlengo wa kuongeza tija kwenye elimu suala la walimu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi limekuwa ni kikwazo kikubwa.

Wakati huo huo wanafunzi waliopata nafasi ya kushiriki uzinduzi wamesema, kitendo cha walimu kuwataka wanafunzi  kimapenzi si cha kiungwana kwani huwatazama kama wazazi  ama walezi.