Jumatano , 29th Apr , 2015

Walimu wa shule ya msingi Hoho iliyopo manispaa ya Iringa katika kata ya itamba leo wamelazimika kusitisha masomo kufuatia walimu kutishiwa amani na wananchi wa kata hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Demetric Mgohamwende amesema kuwa hali hiyo imetokea kufuatia walimu hao kuzuia wananchi kukata miti katika msitu wa shule hiyo kwa ajili ya kuchoma mkaa.

Mwalimu huyo amesema kuwa walifanikiwa kumkamata mmoja kati ya waliokuwa wakihusika kukata miti hiyo ambaye baada ya kukamatwa alimjeruhi mkuu wa shule kwa panga maeneo ya kichwani.

Hata hivyo mkuu huyo ameeleza kuwa kijana huyo alifikishwa katika kituo cha polisi baada ya tukio hilo lakini cha kushangaza amepewa dhamana wakati mkuu huyo akiwa hajatoa maelezo yoyote juu ya tukio hilo hali inayochangia kusababisha walimu wa shule hiyo kupewa vitisho baada ya mtuhumiwa huyo kupewa dhamana.

Aidha akijibia suala hilo Afisa Elimu Manispaa ya Iringa Halfan Omary amesema kuwa tayari wameshapata mashitaka hayo na yamefikishwa kwa mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wa walimu hao na tayari ameshatuma mwanasheria ambaye anafuatilia suala hilo.