Jumatatu , 3rd Jan , 2022

Wakuu wa shule wilayani Mbogwe mkoani Geita ililazimika wapigwe marufuku kuvaa suti mpaka watakapokamilisha vyumba vya madarasa 75 katika shule 16 za sekondari ambapo kwa wilaya hiyo walipokea shilingi bilioni 1.5 na kubakisha chenji ya shilingi milioni 4.

Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Mhandisi Charles Kabeho

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Mhandisi Charles Kabeho, wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa 75 kwa mkuu wa mkoa wa Geita, na kusema kwamba alilazimika kuwapiga marufuku baada ya wilaya yao kuwa ya mwisho kwenye maendeleo ya utekeleaji wa miradi hiyo.

Aidha, Kabeho amesema zaidi ya wanafunzi 4000 wanaotarajia kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka huu wa 2022.