
Makonda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi wa Mkata wilayani Handeni Mkoani Tanga akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili Mkoani hapa na kuongeza kuwa Ma DC hao watambue kufanya hivyo ni kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu .
Alisema Rais anakazi kubwa ya kutafuta pesa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo na chama kina wajibu wa kusimamia watumishi watakaojaribu kutumia vibaya pesa za Serikali.
"Mwacheni Mama akatafute pesa kwa ajili ya maendeleo ya Nchi na sisi kazi yetu kushughulika na watendaji wazembe wanaokula pesa za Serikali "Alisema Makonda
"Hatufanyi haya mambo kwakuwa tunaelekea kwenye uchaguzi hivi karibuni tunafanya kwajili ya wananchi na wewe kiongozi ukitudanganya kama chama tutakula sahani moja na wewe tunataka wananchi wawe naimani na chama chao ukiahidi kutekeleza jambo kwa wananchi unapaswa kutekeleza,"alisisitiza Makonda.