Jumatatu , 11th Aug , 2014

Wakuu wa mkoa 17 ya Tanzania bara waliopatiwa elimu juu ya kupambana na maafa wametakiwa kuifikiasha elimu hiyo kwa wananchi.

Mwenyekiti wa umoja wa wakuu wa mikoa nchini Tanzania, mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Hatua hiyo imetajwa kuwa ni mikakati ya tume ya Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuelimisha jamii kujihami na maafa ya nguvu za asili kwa kupunguza madhara.

Akizungumza na East Africa Radio Mjini Dodoma , Mratibu wa Mafunzo na Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho, amesema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa wenyeviti wa kamati hiyo ambao ni wakuu wa mikoa hali hiyo itawasaidia wananchi kwa ngazi ya Mkoa, wilaya, kata, hadi kijiji na kupunguza madhara yatokanayo mafuriko na ukame na majanga mengine ya asili.

Aidha kumekuwa na sheria inayosimamia maafa ambayo ni ya mwaka 1990 sheria namba 9 sasa inafanyiwa marekebisho ili kuongeza vifungu vitakavyowabana watu ambao wapo katika maeneo ambayo wanaweza kupata mafuriko na kuwaondoa kwa mujibu wa sheria hiyo itakavyo rekebishwa.