Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi.
Akizungumza katika mkutano wa wanahisa wa benki ya wananchi Njombe (Njocoba) mkoa wa Njombe amesema kuwa benki hiyo ni ya wananchi mkoa huo hivyo halmashauri zinatakiwa kuwa na ushirikiano na benki hiyo ili kuimarisha benki inayo wasaidia wananchi wa halmashauri zao.
Ameitaka benki hiyo kuwalea wakulima wao ambao wanakopa kupitia benki hiyo na hasa kwa kuwapatia elimu ya mikopo ili kukabiliana na tatizo la kutorejesha mikopo kwa wakati.
Amesema kuwa benki inatakiwa kuwa ya tofauti na benki zingine zote na hasa kwa kuwa na dawati la wakulima ili kutoa elimu kwa wakulima wanaokopa mikopo na kujua matumizi sahihi ya mikopo yao.
Awali akisoma taarifa ya benki hiyo mwenyekiti wa bodi Yohana Kalinga, alisema kuwa benki hiyo ina pambana na wadaiwa sugu ambao hawajalejesha mikopo ili kuhakikisha benki hiyo inasonga mbele na kuwa mikopo isiyo rejeshwa huathiri ukuaji wa benki.
Amesema kuwa anaomba halmashauri za mkoa wa Njombe kuwa na ushirikiano na benki hiyo ili kuhakikisha kuwa benki hiyo inaimalisha wananchi wanao jiunga kila siku ka mikopo ya kilimo.