Afisa kilimo kutoka TAHA Lota Simon akiwa na ujumbe wa wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha walipotembelea shamba la mkulima mmoja katika eneo la Olasit
Umuhimu viazi hivyo unatajwa na wataalamu wa lishe kwamba vina kiwango kikubwa cha virutubisho vya Vitamin A, C vinavyosaidia katika kuongeza kiwango cha damu katika mwili wa mwanadamu pamoja na kuondoa uwezekano wa kukumbwa na matatizo ya utapiamlo.
Afisa kilimo kutoka TAHA Lota Simon ameuambia ujumbe wa wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha walipotembelea shamba la mkulima mmoja katika eneo la Olasiti nje kidogo ya Jiji hilo kwamba mahitaji ya zao hilo katika nchi ya Israel umewafanya pia kufanya mazungumzo na jeshi la kujenga Taifa JKT kuona uwezekano wa kuongeza uzalishaji wa zao la Viazi ili kukidhi mahitaji ya soko.
Takribani wakulima Mia saba wamejengewa uwezo na TAHA ili kuweza kuzalisha Viazi lishe ambapo baadhi ya wataalamu wa Afya na lishe wametoa mwito kwa wakulima kubadilika na kuona umuhimu wa kulima mazao aina ya mbogamboga yanayoonekana kuwa na soko kubwa.
Ni zao linalotajwa kustahilimili hali yoyote ya hewa kuanzia mwinuko wa mita elfu moja hadi elfu mbili kutoka usawa wa bahari ambapo kwa muda sasa taasisi ya TAHA imekuwa katika harakati za kuendeleza mifumo ya kilimo cha mbogamboga na matunda ambacho licha ya kuchukua eneo dogo la Ardhi kimekuwa na matokeo makubwa kwa wakulima kutokana na upatikanaji wa soko la uhakika.