Wakulima wa mahindi mkoa wa Arusha wameitaka serikali iwasimamie mawakala waliopata zabuni ya kununua mahindi kwa wakulima wayanunue moja kwa moja kwa wakulima hao na si kwa wafanya biashara kama wanavyofanya sasa kitu ambacho kinawafanya wakulima hao kurudi nyuma kimaendeleo.
Wakizungumza watendaji wa Mtandao wa wakulima mkoani Arusha MVIWATA wakulima hao wamesema wanashindwa kupata faida ya kilimo chao kutokana na madalali pamoja na watu wa kati kuingilia kununua mahindi kwa wafanyabiashara badala kwenda moja kwa moja kwa wakulima.
Wakulima hao wametaka serikali ichukua hatua maramoja kuwaondoa madalali hao na watu wa kati na ijuhusishe moja kwa moja katika ununuzi wa mazao yao kwa kuwa watu hao wanawagandamiza kwa kununua mazao hayo kwa bei ya chini na kwenda kuuza kwa bei ya juu zaidi.
Kwa upande wao Wanunuzi wa mahindi hayo kutoka kwa Wafanyabiashara wameitupia lawama serikali na kuitaka iweke mfumo madhubuti ambao utawafanya waweze kwenda moja kwa moja kwa wakulima na sio kupitia kwa mawakala au mdalali.
Katika hatua nyingine, serikali za Tanzania na India zimetiliana saini mkataba wa makubaliano ya kujenga kituo cha Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika chuo kikuu cha Nelson Mandela kilichopo jijini Arusha.
Akiongea mara baada ya kutiliana saini kwa makubaliano hayo jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa amesema kwa kutumia kituo hicho pia kitasaidia kufundishia wanafunzi wa vyuo vikuu katika masomo ya Sayansi na teknolojia na kitajengwa pia tika chuo cha DIT
Aidha amesema kwa kutumia kituo hicho watafiti wa hapa nchini kitawasaidia kufanya utafiti wao wa masuala mbali mbali ya kisayansi kwa kutumia mitambo ya kisasa na matokeo ya tafiti hizo kufanyiwa kazi kwa manufaa ya wananchi.