Alhamisi , 2nd Jun , 2016

Wakazi wa kijiji cha Izumbwe, kata ya Igale Wilayani Mbeya wamelazimika kukodi jengo ili litumike kama Zahanati baada ya Zahanati ya awali kuteketea kwa moto zaidi ya Miezi mitatu iliyopita.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala

Wakizungumza na East Afrika Radio wakazi wa kijiji hicho wamesema kuwa walifikia uamuzi wa Kuchangishana fedha kwa ajili ya Kukodi jengo hilo ili waendelee kupata huduma ya Afya.

Wamesema pamoja na kukodi jengo hilo bado wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Dawa pamoja na wauguzi.

Diwani wa kata hiyo Mmichael Mwasombe amesema baada ya Zahanati ya Kijiji cha Izumbwe kuteketea kwa moto, waliazimia kuhamishia huduma za afya kwenye nyumba ya kuhifadhia mazao ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo.