
Wakizungumza na East Africa Radio wakazi hao wamesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya nchi barabara hiyo isipofanyiwa jitihada za kukarabatiwa inaweza kusababisha kukosekana kwa mawasiliano kati ya wakazi wa Boko na Magereza na wale wa Bunju na Tegeta.
Wamesema kundi la vijana wanaochimba michanga pembezoni mwa barabara hiyo ndio chanzo cha kuendelea kuharibika kwa barabara hiyo, huku serikali ya mtaa ikichukua ushuru kwa malori yanayokwenda kubeba michanga hiyo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa huo Bi. Judith Joseph akizungumzia tatizo hilo amesema kwa sasa hakuna bajeti ya fedha kwa ajili ya kukarabati barabara hiyo na amekanusha kuwepo kwa watu wanaochukua fedha kama ushuru kwa malori yanayokwenda kubeba michanga.