Jumatano , 16th Mar , 2016

Zaidi ya Hekta 3827 za zao la Mpunga zimeharibiwa na ndege aina ya kwereakwerea wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza kata ya Kijima, Mabuki na Ilijumate hali inayotishia baa la njaa katika wilaya hiyo.

Moja ya Mashamba ya Mpunga

Kufuatia hali Mkuu wa Wilaya Mwajuma Nyiluka amesema kuwa msaada wa haraka kutoka serikalini unahitajika ili kunusuru wakulima wa kata hizo dhidi ya tishio hilo la baa la njaa ambalo linawanyemelea.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa malengo waliyojiwekea katika wilaya hiyo ya kupata zaidi ya tani elfu saba itashindikana kutokana na athari za ndege hao hali inayosababisha tahariki katika Wilaya hiyo.

Wakulima hao ambao wengi wao sasa wamehamia mashambani kwa ajili ya ulinzi ikiwemo kufanya mbinu za ulinzi wa asili wa mashamba lakini lakini idadi hiyo kubwa ya ndege hayo inawawia vigumu kulinda mazao yao

Aidha athari za Ndege hao pia zimeathiri mahudhurio ya wanafunzi wa kata hizo shuleni baada ya wanafunzi hao kuhamia mashambani na wazazi wao kwa ajili ya kusaidia kulinda mashamba hayo ya mpunga hali inayowafanywa washindwe kwenda shule.