Jumanne , 13th Mei , 2014

Wakazi wa Makongo Juu Kata ya Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wameilalamikia serikali kwa kufumbia macho tatizo la ubovu wa barabara kati ya eneo la survey na makongo juu, hali inayochangia kukosekana kwa usafiri wa umma wa uhakika.

Moja ya barabara za Makongo katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa katika hali mbaya.

Sehemu ya barabara hiyo ambayo ina urefu wa Kilometa 6 tu ni ya vumbi na yenye mashimo ambayo mengi yamesababishwa na ubovu wa miundombinu imeibua adha ya usafiri wa kwa wakaze hao kutokana na kutokuwepo kwa daladala za kuwasafirisha.

Wakizungumza na East Africa Radio kwa nyakati tofauti wakazi hao wameeleza kuwa hali hiyo imedumu kwa kipindi kirefu sasa kutokana na ubovu wa arabara na kuwafanya wamiliki wa mabasi kutosajili mabasi yao
kwa ruti ya Makongo Juu.

Naye mmoja wa dereva wa gari ziendazo na Makongo Juu pamoja na mpiga debe wa Sudi Mohamedi hawakusita kuongea kuhusu kero wapatazo kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Mbali na wakazi wa Makongo Juu kukumbwa na kero hiyo ya usafiri kumekuwepo na tatizo la upatikanaji wa maji safi, licha ya kuwepo na mradi wa wa mambomba ya maji uliowekwa na wataalamu kutoka China mwaka
2009, bado maji hayatoki katika mabomba hayo.