
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Njombe Eluminata Mwenda
Ombi hilo limetolewa na wakazi hao wakati wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo ya mabondeni walipo tembelewa na kituo hiki huku zikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa zoezi la bomoa bomoa ambapo wanahitajiwa kubomoa wao wenyewe kabla ya halmashauri haijapitisha tingatinga maeneo hayo.
Halmashauri hiyo mnamo Januari 4 ilitoa tangazo la kuwataka wakazi waliojenga maeneo ambayo yapo chini ya mita 60 toka bonde ama eneo la wazi na maeneo Owevu kutoka siku 30 kutoka tarehe ya tangazo kubomoa weyewe nyumba zao kala ya halmashauri kubomoa.
Wananchi hao wameomba kuongezewa muda ili waweze kupata muda wa kutosha kuhakikisha kuwa wanabomoa na kupata maeneo ya kuhamia.
Kituo hiki kimeshuhudia wananchi wakiendelea na maisha yao ya kila siku huku zikiwa zimebaki siku kufikia siki 30.
Hata hivyo halmashauri imesema kuwa kwa watakaoiachia halmashauri hiyo kubomoa basi itahakikisha kuwa gharama za ubomoaji zitarejeshwa na mwenyenyumba baada ya kubomoa.
Hata hivyo Mkurugenzi Eluminata Mwenda hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo.