Jumatatu , 28th Apr , 2014

Maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wanahitaji msaada wa dharura, kutokana na kukumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo mpaka sasa watu saba wamekwishafariki dunia kutokana na mafuriko hayo.

Mbunge wa jimbo la Kyela mkoani Mbeya, Dkt Harrison Mwakyembe

Kutokana na athari hizo kwa wakazi wa Wilaya hiyo uongozi wa Wilaya hiyo ukiongozwa na Mbunge wa Kyela Dkt. Harrison Mwakyembe ameomba msaada kutoka katika makampuni mbalimbali nchini kutoa misaada ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika Wilaya hiyo.

Dkt.Mwakyembe amesema wakazi hao wameathirika kwa kiasi kikubwa ambapo kwa sasa wanahitaji msaada wa Chakula,Mavazi na sehemu ya kujihifadhi wakati wakianza utaratibu wa kukarabati Nyumba zao.