Alhamisi , 14th Jan , 2016

Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi nchini kuungana na wakandarasi wa nje ili waongeze ujuzi na uzoefu na kuleta ufanisi katika shughuli za uendelezaji miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwini Ngonyani

Waziri mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la miundombinu baina ya wakandarasi wa ndani na nje na kuongeza kuwa kwakuwa wakandarasi wa nje wana uzoefu wa muda mrefu watawasaidia wale wa ndani kujifunza vitu vingi na baadaye kuendeleza miradi mikubwa itakayoachwa na wakandarasi wa nje.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwini Ngonyani amewataka wakandarasi wa ndani kushindana na wale wa nje ili kukuza soko lao ndani na nje ya nchi.

Aidha Mhandisi Ngoyani ameongeza kuwa wakandarasi watanzania watanufaika na miradi mikubwa ya barabara za juu ambayo itaanza hivi karibuni ambazo zitasaidia kupunguza foleni katika Jiji la Dar es salaam.