Jumatano , 4th Oct , 2023

Takriban watu 400 nchini Misri wamekamatwa kutokana na "matukio ya ghasia" baada ya Rais Abdul Fattah al-Sisi kutangaza kwamba atawania muhula wa tatu, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Uchaguzi wa rais nchini Misri umepangwa kufanyika mwezi Disemba.

 

Matamshi ya Rais Sisi siku ya Jumanne yaliibua hasira ya umma  video za mitandao ya kijamii ziliteka maandamano katika mji wa kaskazini magharibi wa Marsa Matrouh.

Katika kanda hiyo ya video, watu wanaweza kusikika wakiimba "Sisi nje" na kutoa wito kwa utawala wake wa muongo mmoja kuanguka. Video nyingine zilionyesha mapigano kati ya waandamanaji na polisi.

Tovuti ya habari ya Al-Manassa inayomilikiwa na watu binafsi ilimnukuu Saleh Abou-Attiya, katibu mkuu wa chama cha Marsa Matrouh Bar Association, akisema kuwa watu 400, wengi wao wakiwa "vijana", walikuwa wamezuiliwa.

Mkuu huyo wa zamani wa jeshi amekuwa madarakani tangu aliposaidia kumuondoa madarakani Mohammed Morsi, kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood, mwaka 2013, wakati kukiwa na maandamano makubwa dhidi ya utawala wake.

Wanaharakati wanasema muhula wa rais Sisi madarakani umegubikwa na ukandamizaji wa kikatili wa wapinzani wote na kuporomoka kwa uchumi wa Misri.

Uchaguzi wa rais nchini Misri umepangwa kufanyika mwezi Disemba.