
Eneo la Machimbo ya Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni Dar es Salaam
Katika ajali hiyo, watu wengine wawili wameokolewa wakiwa hai baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo hayo ya mawe ya Kikikaka, Mjimwema Kigamboni Dar es salaam. Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjimwema, Mohamed Gharib Mohamed amethibitisha na kusema majeruhi wamekimbizwa hospitali. Kwamjibu wa Mwenyekiti wa mtaa huo, ajali hiyo imetokea mapema leo Aprili 3, 2022 saa tatu asubuhi.