Alhamisi , 11th Aug , 2022

Jumla ya Wahamiaji haramu 47 raia wa Ethiopia na Somalia  wamekanatwa mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria 

Wahamiaji hao wamekamatwa usiku wa kuamkia leo Agosti 11, 2022 saa 9 usiku wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo inaelezwa walikuwa wakielekea nchini Afrika Kusini na Malawi 

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyeki wa ulinzi na usalama Nurdini Babu ameipongeza idara ya uhamiaji pamoja na jeshi la polisi  kwa kushirikiana vyema katika kuhakikisha mkoa wa Kilimanjaro unakua salama ikiwa ni pamoja na kuwabaini wahamiaji haramu wanaoingia kinyemela bila kufuata kanuni na taratibu

Akizungumza wakati wa ushushwaji wa wahamiaji hao haramu amesema wahamiaji hawakatazwi ila sio wahamiaji haramu na nchi ya Tanzania ni huru hivyo sheria na kanuni za uhamiaji ni vyema zikafuatwa.

Idara ya uhamiaji mkoani Kilimanjaro  ikishirikiana na kamanda wa jeshi la polisi mkoa imeendesha oparesheni maalum katika mpaka wa Tanzania na Kenya iliyofanikisha kuwkaamata wahamiaji hao

Mkuu wa uhamiaji mkoani Kilimanjaro Edward Mwenda amewaambia waandishi wa Habari kuwa oparesheni hiyo inalenga kutokomeza wahamiaji hao kutumia Tanzania kama uchochoro