
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
Waziri Masauni ameyasema hayo leo Septemba 3, 2023, jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kituo cha Polisi Mavurunza, Wilaya ya Kipolisi Kimara, wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, ambacho hadi kukamilika kwake kimegharimu shilingi million 100 huku wananchi wa Mtaa huo wakichangia shilingi milioni 70.
"Niwahakikishie, hakuna mhalifu atakayevuka katika mipaka ya Jeshi la Polisi, hatushindwi, hivi juzi Mkoani Njombe ‘walitubipu’ shughuli yao imeisha usiku wa leo, Jeshi la Polisi na Makamanda ni imara na wananchi wanaonesha mshikamano katika kipindi hiki chenye shughuli nyingi za kiuchumi, Dar es Salaam ni tulivu, Tanzania ni salama." amesema Masauni.
Hata hivyo, Waziri Masauni amelitaka Jeshi hilo kutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuhakikisha haki inatolewa sambamba na kushughulikia kero za wananchi kwa haraka na kwa weledi.
"Najua wapo baadhi ya askari nchini wanafanya mambo kinyume na kanuni za Jeshi la Polisi, Jeshi linafuatilia na kuwachukulia hatua, na pia kwa upande wa serikali baada ya malalamiko ya wananchi Rais Samia Suluhu Hassan aliunda Kamati ya Tume ya Haki Jinai kuangalia nini kifanyike ili kuimarisha zaidi Jeshi la Polisi," amesema Waziri Masauni.