Jumatano , 29th Jul , 2020

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kivule iliyopo Manispaa ya Ilala Dk.Thobias Mboto amesema tangu kuanzishwa Hospitali hiyo Juni 3, mwaka 2020 hadi sasa zaidi ya wagonjwa 1,500 wameshatibiwa.

Pichani ni wakati wa ujenzi wa hospitali ya Kivule. Picha na Maktaba

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kivule iliyopo Manispaa ya Ilala Dk.Thobias Mboto amesema tangu kuanzishwa Hospitali hiyo Juni 3, mwaka 2020 hadi sasa zaidi ya wagonjwa 1,500 wameshatibiwa.

Akitoa Taarifa hiyo Dokta Mboto amesema Hospitali hiyo ya Wilaya tayari imekwisha toa huduma kwa wakinamama zaidi ya 50 ambao wamejifungulia hospitalini hapo wakitoa huduma kwa wananchi kwa saa 24 yani usiku na mchana ikihudumia Wakazi wa Kivule, Kitunda, Gongolamboto na maeneo mengine.

Amesema Mara baada ya kuanzishwa kwa hospital hiyo imekuwa msaada mkubwa kutokana na mwitikio kuwa mkubwa huku akitoa wito kwa Wananchi wanaozunguka maeneo hayo kuwa walinzi wa miundombinu hiyo ambayo serikali imewekeza hapo gharama kubwa akibaisha pia kuanza kwa huduma ya Bima Mara baada ya baadhi ya Taratibu kukamilika.

Hospitali ya Wilaya Kivule iliyopo Manispaa ya Ilala ni miongoni mwa hospital mpya ambayo serikali imezijenga kwa Jiji la Dar es Salaam ikigharimu zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni 500.