Ijumaa , 6th Sep , 2024

Waganga wa Tiba asili waomba kutohusishwa na matukio ya ukatili yanayotokea kwenye jamii kwani wao hawahusiki na kuwatuma watu wafanye ukatili badala yake wameomba kupewa thamani kama ambavyo madaktari wa Hospitalini.

Mganga wa tiba asili.

Waganga wamesema wanataka kuthaminiwa kama madaktari wa hospitali, kwani dawa zote za hospitali zilitokana na dawa za asili zikaboreshwa ndio zikatumika Hospitali.

Wamesema vitendo vingi wamekuwa wakitajwa lakini sio kweli kama wanatumika isipokuwa watu wamekosa utu ndio maana wanatekeleza matukio hayo.