Jumatano , 30th Mar , 2022

Waganga wa tiba asili mkoani Katavi wameaswa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuwabaini wahalifu wa ujambazi.

Mkuu wa Polisi Wilayani Mlele Mkoani hapa OCD Anthony Gwandu

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo Mkuu wa Polisi Wilayani Mlele Mkoani hapa OCD Anthony Gwandu aliwaomba waganga hao kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini wahalifu.

OCD Gwandu ameyasema hayo wakati wa uhitimishaji wa mafunzo na utoaji vibali kwa waganga wa tiba asili, mafunzo yaliyoendeshwa na Chama cha waganga na wakunga wa tiba asili Tanzania (TADTM) yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyagwida Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.

Tazama Video hapo chini