Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Waficha maiti kuepuka gharama za kupeleka mochwari

Jumamosi , 17th Jul , 2021

Wananchi wa Kijiji na Kata ya Lupanga, wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamesema wamekuwa wakilazimika kuficha maiti, kuzuia matangazo na kujizuia kulia unapotokea msiba jioni au mchana majumbani mwao ili kuepuka gharama za kusafirisha maiti kwenda mochwari.

Miguu

Wananchi wa Kijiji hicho wameeleza changamoto hiyo katika mkutano wao na mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga, alipofika katika Kijiji hicho ikiwa ni ziara yake anayoifanya katika kila Kijiji ili kupata changamoto na kuzifanyia kazi.

Zebedayo Mgaya ni mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho aliyeeleza changamoto hiyo huku akibainisha kuwa hivi karibuni alifiwa na ndugu yake na kulazimika kukaa kimya na maiti nyumbani kwake akihofia kutangaza kwa kuwa uongozi wa Kijiji hicho ungemtaka kufikisha mwili wa marehemu mochwari iliyopo umbali wa zaidi ya Km 10 kutoka kwenye kijiji hicho huku gharama za usafirishaji pekee zikiwa ni shilingi 40,000 hadi 50,000.

"Gharama za kusafirisha mwili kutoka hapa mpaka mochwari iliyopo Mlangali ni zaidi ya Km 10 na gharama zake ni 50,000 na sijui kwanini gharama ya kusafirisha maiti ni kubwa kuliko kusafirisha mahindi, nashauri kama Mochwari ni mradi mzuri kwa Wizara ya Afya au Halmashauri basi wajenge kila kijiji mahali ambapo mtu anaweza kufikisha maiti na kurudisha nyumbani, "amesema  Zebedayo Mgaya.

Aidha, wananchi wa kijiji hicho wamesema wamekuwa na hofu wanapopata msiba na kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji kwa kuwa imekuwa ikiwalazimu kufikisha maiti katika mochwari kutokana na kutoruhusiwa kulala na maiti huku wengi wao wakiwa hawana ada ya mochwari kwa wakati huo.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Baraka Mfaume, aliyeongozana na mbunge katika mkutano huo amesema chama kimepokea changamoto hiyo na kuelekeza ofisi ya mkuu wa wilaya kuifanyia

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali