Alhamisi , 23rd Apr , 2015

Kilele cha maadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yanataraji kufanyika Aprili 28 mwaka huu jijini Arusha ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele hicho.

Mmoja wa wafanyakazi wa Ndani.

Katika kuazimisha maadhimisho hayo Wafanyakazi waonaojihusisha na suala la usafi katika maeneo mbalimbali wametakiwa kuwadai vitendea kazi waajiri wao.

Katibu wa chama cha wafanyakazi wa majumbani na hotelini (CHODAWU) Bw. Slyvester Mshana amesema kumekuwa na ukiukwaji wa makubaliano baina ya pande zote mbili kwa muajiri na muajiriwa.

Amesema waajiri wawe makini kwa wafanyakazi wanaoshindwa kutumia vitendea kazi kama (gloves) kwani yakitokea madhara gharama hizo zitamuhusu muajiri mwenyewe kumtibu mfanyakazi wake.

Hata hivyo amesema wao kama muungano wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi wameona kuna ukiukwaji wa hali ya afya na usalama kazini hususani watu wanaofanya usafi katika maeneo mbalimbali mkoani Iringa na kuwataka wajiunge na vyama vya kazi.