Jumanne , 29th Apr , 2014

Katika kuelekea sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, baadhi ya wafanyakazi kutoka katika sekta mbalimbali zilizo za serikali na zisizo za serikali nchini Tanzania wamelalamikia mishahara midogo isiyoendana na ukali wa maisha.

Waziri wa kazi na ajira nchini Tanzania, Bi.Gaudensia Kabaka

Wakizungumza leo na EATV, wafanyakazi hao wameitaka serikali kuacha kutoa ahadi zisizotekelezeka na badala yake waboreshe mishahara ya wafanyakazi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Aidha,wameitaka serikali kupunguza kodi wanayokatwa wafanyakazi katika mishahara yao sambamba na kuhakikisha kwamba mfanyakazi anakuwa na maisha bora yatakayomwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.