
Pamoja na Kim na Putin kuwa marafiki, picha za jana Jumatano zimeonyesha hatua za ajabu za jambo hilo kuficha dalili zozote kuhusu afya ya Kim. Katika chapisho kwenye Telegram, ripota wa Kremlin Alexander Yunashev alishiriki video ya wafanyakazi wawili wa Kim wakisafisha kwa uangalifu chumba katika mji mkuu wa China, Beijing ambapo Kim na Putin walikutana kwa zaidi ya saa mbili.
Sehemu ya nyuma ya kiti na sehemu za kuwekea mikono zilisuguliwa na meza ya kahawa karibu na kiti cha Kim pia ilisafishwa. Glasi ya kunywea ya Kim pia iliondolewa. "Baada ya mazungumzo kukamilika, wafanyakazi walioandamana na mkuu wa DPRK waliharibu kwa uangalifu alama zote za uwepo wa Kim," mwandishi huyo alisema, akimaanisha Korea Kaskazini.
Nalo gazeti la Nikkei la Japan limeripoti, likinukuu mashirika ya kijasusi ya Korea Kusini na Japan kwa kusema kuwa kama ilivyo katika safari za awali za nje, Kim alipaki choo chake kwenye treni yenye saini ya kijani iliyompeleka Beijing kuficha dalili za kiafya.
Hatua hizo ni itifaki ya kawaida tangu enzi za mtangulizi wa Kim, babake Kim Jong Il, kwa mujibu wa Michael Madden, mtaalamu wa uongozi wa Korea Kaskazini katika Kituo cha Stimson chenye makao yake nchini Marekani.
Mnamo mwaka wa 2019, baada ya mkutano wa kilele wa Hanoi na Rais wa Marekani, Donald Trump, walinzi wa Kim walionekana wakizuia sakafu ya chumba chake cha hoteli na kusafisha chumba kwa masaa, na kutoa vitu pamoja na godoro la kitanda. Timu ya Kim imeonekana kusafisha vitu kwa uangalifu kabla ya kuvitumia pia.
Wakati wa mkutano wake wa 2018 na Rais wa wakati huo wa Korea Kusini, Moon Jae-in, walinzi wa Korea Kaskazini walinyunyiza kiti na dawati pamoja na sanitizer na kuifuta kabla ya Kim kuja kuketi.
Kabla ya kuketi kwenye mkutano mwingine wa kilele na Putin mnamo 2023, timu yake ya usalama ilifuta kiti chake kwa dawa, na kukagua kwa nguvu kuhakikisha kiti kiko salama, huku mmoja wa walinzi akitumia detector ya chuma kukagua kiti, picha za video zilionyesha.