Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Dkt Abdallah Kigoda.
Akizungumza na wafanyabiashara Mkoani Morogoro Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja, amesema bado wanaendelea na mazungumzo na Serikali kupita Mamlaka ya Mapato nchi TRA, kuhusu mfumo mzima wa kodi ili uweze kusaidia mashine za kutolea risit kwa njia ya elektroniki EFD.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanayabiashara Mkoani Morogoro Bw. Ally Mamba amesema Wafanyabiashara wa mkoa huo kuwa wako tayari kutumia mashine za EFD, iwapo mfumo huo wa uksanyaji wa kodi utarekebishwa huku akitoa wito wa kuwa wamoja katika kutatua matatizo yanayowakabili.
Wakati huo huo, serikali ya Tanzania imesema sasa inaweza kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kutokana na kuzinduliwa kwa mawasiliano ya Video ambapo viongozi watalazimika kutumia mawasiliano hayo badala ya kwenda moja kwa moja katika eneo la tukio.
Akiongea jijini Dar es salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa mawasiliano hayo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema viongozi hawatalazimika kwenda kwenye mikutano badala yake watatumia mawasiliano hayo yanayojulikana kama Video Comference kuongea moja kwa moja na wahusika mahala walipo.
Profesa Mbarawa amesema safari za baadhi ya viongozi zimekuwa zikiigharimu serikali hivyo kupitia Video Conference hakutakuwa na ulazima kwao isipokuwa kama watahitajika kufanya hivyo.