Ijumaa , 22nd Mei , 2015

Halmashauri ya Jiji la Tanga imesema ni lazima wafanyabiashara wote kufuata kanuni na sheria zilizowekwa kwenye kila Soko kwa kuuza bidhaa husika inayotakiwa katika kila soko kwa namna walivyokubaliana.

Wakazi wa jiji la Tanga wakichagua maembe katika Soko la Masiwani Chuma.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Biashara wa Jiji la Tanga,Dawson Mongi wakati alipozungumza na kituo hiki ofisini kwake na kusema kuwa wafanyabiashara wamekuWa wakikiuka taratibu zilizopangwa na kufanya biashara hovyo.

Dawson amesema kabla ya kuamua kuchukua hatua waliwaita wafanyabiashara na kukaa na kuzungumza na sheria, wao ndiyo waliziafiki na kuamua kutenganisha kila bidhaa kukaa katika soko lililopangwa ili kupunguza msongamano kwa wakazi wa jiji.

Amesema watawachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na faini baada ya kukiuka utaratibu kutokana na makubaliano ambayo walishaafiki.