Dkt. Kijaji ameyuasema hayo Bungeni Dodoma kufuatia swali la Mbunge wa Viti Maalumu Neema Mgaya aliyetaka kujua changamoto za mtandao wakati wa matumizi ya ya EFD ambazo zinaweza kusababisha mtu ashinde kupata risiti.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri amesema serikali imejipanga kufanya marekebisho katika eneo hilo na akatumia fursa hiyo katika kuwataka wafanyabiashara jijini Dar es salaam waende kwenye mamlaka ya mapato kuchukua mashine za EFD.
Wafanyabiashara wenye mitaji ya milioni 14 hadi 20 wanatakiwa wakachukue mashine kwa kuwa mashine zilizoingiz\wa ni 5,703 na mpaka leo wafanyabiashara 118 tu ndiyo waliochukua mashine hizo.
Aidha Naibu Waziri amesema nia ya serikali ni kuhakikish mashine za EFD zinapelekwa nchi nzima ili serikali iweze kupata mapato ya kuendesha shughuli za maendeleo.

