
Wakizungumza na #EATV wafanyabiashara hao waliofika sokoni hapo leo wamesema kitendo hicho kimesababisha kuwakwamisha kufanya biashara hiyo kutokana na kutotarajia kupanda ghafla kwa bei ya nyanya katika soko hilo
Nao wafanyabiashara wa nyanya za jumla katika soko hilo la Temeke Stereo wamesema kupanda kwa bei ya nyanya kumetokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo ya vijijini zinakotoka nyanya hizo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitengo cha nyanya katika soko hilo Banzi Kaunda amesema hiyo ni hali ya kawaida kutokea jambo ambalo wafanyabiashara hao wa nyanya za rejareja wanapaswa kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki