Jumanne , 7th Jun , 2016

Wafanyabiashara nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia ubora katika ufungashaji wa biadhaa zao ili waweze kuendana na ushindani wa soko la kimataifa.

Wafanyabiashara nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia ubora katika ufungashaji wa biadhaa zao ili waweze kuendana na ushindani wa soko la kimataifa.

Wito huo umetolewa na mweka hazina wa soko la Magomeni Bw Yusuph Waziri kwenye mahojiano maalum na East Africa Radio na kubainisha kuwa kwa hivi sasa wafanyabiashara wengi husuasani wa viazi mbatata wanakwenda kununua viazi nchini kenya kwa sababu vinafungashwa vizuri na hamna uwezekano wa kukuta viazi visivyofaa kwa matumizi.

Aidha ubora wa viazi vya kenya ni tofauti sana na viazi vinavyozalishwa nchini Tanzania kwani viazi hivyo vinakuwa vikubwa zaidi na vinamuonekano mzuri ukilinganisha na viazi vya hapa nchini.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa viazi katika soko la Magomeni wamesema kuwa wanalazimika kwenda kununua kenya sababau kule bado wanaruhusu lumbesa wakati hapa nyumbani hawaruhusu lumbesa hali inayowapelekea wafanyabiashara hao kupata faida ndogo.